Upeo Studio Ni kitovu cha ubunifu kinachotengeneza maudhui ya kidigitali kwa kutumia teknolojia ya Akili MNEMBA (AI). Tunajivunia kutunga na kuimba nyimbo za aina zote kwa lugha mbalimbali ikiwemo nyimbo za watoto za kujifunza, pamoja na kutengeneza filamu za AI zenye hadithi za kusisimua na mafunzo ya kina.Tunaleta mapinduzi katika tasnia ya muziki na filamu kwa kuchanganya ubunifu wa kibinadamu na nguvu ya teknolojia ya kisasa. Lengo letu ni kuburudisha, kuelimisha, na kuhamasisha hadhira yetu kupitia kazi za sanaa zinazovutia na zenye maudhui bora kwa watoto na watu wa rika zote.
WAIMBAJI WETU NI HURI NA TULI . HURI NA TULI SIYO WATU HALISI BALI WAMETENGENEZWA KWA AKILI MNEMBA. HURI NI MWANAUME NA TULI NI MWANAMKE. SURA ZAO NDIYO HIZO UNAZOZIONA KWENYE PICHA, NAZO ZIMETENGENEZWA KWA AI.


01.
Huduma Zetu
MUZIKI AINA ZOTE
Tunatunga na kuimba nyimbo nzuri aina zote kwa kutumia Akili Mnemba (AI). Nyimbo hizo ni kama vile nyimbo za sherehe, harusi, kampeni, Injili, jubilee, michezo, matamasha, mtu binafis, kikundi ama taasisi nk. Tunaimba aina zote za muziki kama vile Bongofleva, Rnb, Afrobeat, reggae, amapiano, taarab, hip hop, injili nk. kwa kutumia lugha mbalimbali ikiwemo Kiswahili, Kiingereza, Kihindi, Kifaransa nk.
NYIMBO ZA WATOTO
Tunawaletea nyimbo za watoto za kujifunza, zikitengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba (AI). Tunaunda nyimbo zenye burudani na mafunzo, zikilenga kusaidia watoto kujifunza kwa urahisi kupitia muziki wa kuvutia na wa kisasa. Kuanzia herufi, namba, hadithi za maadili hadi nyimbo za ubunifu, tunahakikisha kila wimbo unakuza uelewa na hamasa ya kujifunza kwa watoto.
FILAMU
Tunabadilisha tasnia ya burudani kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba (AI). Tunatengeneza filamu za AI zenye hadithi za kusisimua, ubunifu wa hali ya juu, na uhalisia wa kipekee. Kila filamu tunayounda inalenga kuburudisha, kuelimisha, na kuleta maudhui ya kisasa kwa hadhira ya Afrika na dunia nzima.
Subscribers
Projects
Music Videos
Commercials
02.
Nyimbo
Wimbo unawatambulisha Huri na Tuli
WIMBO: Sisi ni Huri na tuli
Wimbo wa kuelimisha na kuhamasisha masuala ya Ardhi
WIMBO: ARDHI YETU, WAJIBU WETU
Nani amevujisha siri? nani kawasha moto? nani kafanya jambo hili?
WIMBO: AU NI WEWE?

Mfano wa matumizi chanya ya teknolojia
“Hongereni kwa kutuletea nyimbo bora zinazoburudisha na kufundisha! Upeo Studio ni mfano wa matumizi chanya ya teknolojia katika sanaa.”
Sarah N.

Naomba nyimbo zaidi!
“Muziki wenu ni ushahidi kwamba AI inaweza kusaidia sanaa kustawi! Naipenda kazi yenu, Upeo AI Studio. Naomba nyimbo zaidi!”
Kelvin O.

Big up!
“Mnaonyesha kuwa teknolojia inaweza kutumika kuleta ubunifu wenye maana! Nyimbo zenu zinanifanya nitafakari na pia kufurahia. Big up!”
Fatuma L.

Endeleeni kutupeleka mbali!
“Nawapenda sana Huri na Tuli! Muziki wa Upeo AI Studio ni wa kipekee, unafundisha na pia unaburudisha. Endeleeni kutupeleka mbali!”
David S.

Nashukuru kwa kazi nzuri
“Burudani na elimu kwa wakati mmoja! Nyimbo zenu zina ujumbe wenye nguvu na sauti za kuvutia. Nashukuru kwa kazi nzuri!”
Neema J.

Kazi nzuri
“Sijawahi kufikiria AI inaweza kutoa muziki wenye hisia na maana kama huu! Upeo AI Studio mmevunja mipaka ya ubunifu. Kazi nzuri!”
Moses R.

Hongereni sana
“Hakika Upeo AI Studio mmeleta mapinduzi kwenye muziki wa AI! Nyimbo zenu zinagusa moyo na kufundisha kwa njia ya kipekee. Hongereni sana!”
Asha M.

Endeleeni kutupatia ladha hii
Upeo AI Studio mnatoa nyimbo zenye ubunifu wa hali ya juu! Ujumbe mzito, burudani safi, na sauti za Huri na Tuli zinavutia sana. Endeleeni kutupa ladha hii!”
Juma K.
04.
Makala
05.
Je, unatamani tukutungie wimbo wako mzuri?
Ikiwa jibu ni ndiyo, karibu sana. Tunakutungia wimbo wowote utakao mfano: Harusi, send-off, Kumshukuru Mungu, Jubilee, Wimbo wa familia, sherehe za kidini, Wimbo wa ukoo, wimbo wa kumpa zawadi mpenzi wako na kadhalika. Nyimbo zote hizo zitataja majina ya unaotaka watajwe kwenye wimbo huo ( lakini tutahitaji kibali cha wahusika kutaja majina yao). Utachagua sauti ya kike au kiume ndiyo iimbe pia utachagua aina ya muziki kama ni Bongofleva, hip hop amapiano, RnB na kadhalika. Waimbaji wetu HURI na TULI (AI) watafanya kazi zote hizo. Utapata wimbo wako dani ya masaa 24-48 tu. Bofya Contact hapo chini kujaza fomu ya maelezo.
